Kipa wa Blues, Thibaut Courtois, anayecheza kwa mkopo Atletico, amekuwa akizungumziwa na wengi kama mlinda mlango hodari kinda Ulaya, baada ya kudaka vizuri akiwa na klabu hiyo ya Hispania kwa misimu mitatu.

Costa amefunga mabao 19 katika La Liga msimu huu, akishika nafasi ya pili kwa ufungaji nyuma ya Cristiano Ronaldo wa Real.
Kipaumbele cha Mourinho katika usajili huu ni mshambuliaji, na Mreno huyo amegoma kuondoka Januari.
Chelsea ilitaka kipa Courtois asaini Mkataba mpya licha ya kwamba hajawahi kuchezea timu ya Stamford Bridge, lakini Mbelgiji huyo angependa kuchezea klabu kwa Mkataba wa kudumu badala ya mkopo.
Courtois awali alisema atarejea Chelsea tu kuwa kipa namba moja mbele ya Petr Cech.