come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

YANGA KUWAKABILI WAALBANIA LEO.

Na Baraka Kizuguto, Antalya

TIMU ya Yanga leo itashuka dimbani kucheza na timu ya KS Flamurtari Vlore inayoshika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Albania ikiwa ni sehemu ya mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu kwa timu zote, mchezo utakaofanyika katika eneo la Side Manavagat.

Huu utakua ni mchezo wa tatu wa Yanga Africans wa kujipima nguvu dhidi ya timu hiyo ya Ligi Kuu nchini Albania baada ya kuwa imeshacheza michezo miwili na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ankara Sekerspor na 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK.


Kocha mkuu wa Yanga,  Hans van der Pluijm ameendelea na mazoezi jana asubuhi na jioni ataendelea na mazoezi pia kuwaandaa vijana wake kuwa tayari kwa mchezo huo, lakini pia kuwaweka tayari kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.
 
Baada ya mchezo dhidi ya timu KS Flamurtari Vlore, Yanga itakamilisha ziara yake ya kambi ya mafunzo nchini Uturuki kwa kucheza na timu ya Simurq PIK inayoshikri Ligi Kuu nchini Azerbaijan katikati ya wiki ijayo kabla ya kuanza safari ya kurejea nchini Tanzania.

Hali ya hewa jijini Manavgat ni nzuri na sio ya baridi kali kiasi kwamba haiwalazimu wachezaji kuwaa vifaa vya michezo vya baridi kwani hali inawaruhusu kuweza kufanya mazoezi na kucheza bila kuwa na mataitzo yoyote.

Mpaka sasa katika kambi ya klabu ya Yanga nchini Uturuki hakuna mchezaji yoyote majeruhi isipokuwa kiungo Hassan Dilunga ambaye anasumbuliwa na malaria na tayari anaendelea vizuri baada ya kupatiwa tiba na daktari wa timu Dk. Sufiani Juma.