
Ameposti picha akiwa na wachezaji wenzake Alex Song, Carles Puyol na Gerard Pique wakati ndege inataka kuruka mabingwa hao wa Hispania wakienda jiji la Manchester kwa ajili ya mechi ya kwanza ya hatua ya 16 Bora, itakayopigwa Uwanja wa Etihad.
Barcelona inakwenda kwenye mechi hiyo ikitoka kuichapa mabao 6-0 Rayo Vallecano Jumamosi katika La Liga, matokeo ambayo yanawafanya waendelee kukabana koo na Real Madrid na Atletico kileleni.
Lakini watakutana na Manchester City ambayo pia iko vizuri, ikiwa imetoka kuing'oa Chelsea katika Raundi ya Tano ya Kombe la FA mwishoni mwa wiki na kocha Manuel Pellegrini, ambaye ana uzoefu wa kucheza na Barca, anajiamini City inaweza kufanya vizuri katika mchezo huo.