Bayern Munich walijishindia taji lao la 24 la
ligi ya Ujerumani Jumanne kwa ushindi wa 3-1 Hertha Berlin, vijana hao
wa Pep Guardiola wakivunja rekodi kwa kushinda taji hilo wakiwa
wamesalia na mechi saba za kucheza.
Kwenye msimu wake wa kwanza huko, Guardiola sasa ameshinda mataji matatu katika miezi tisa baada ya kushinda Super Cup ya Uefa Agosti mwaka jana na Desemba akashinda Kombe la Dunia la Klabu.
“Nina furaha kwamba hatimaye tumefanikiwa,” alisema Guardiola huku vijana wake wakiweka mwanya wa alama 25 uongozini dhidi ya Borussia Dortmund walio wa pili.
"Haikujalisha ni wakati gani tumelipata lakini bora tu tumeshinda taji hilo ni vyema kwa klabu hii kuu.”
Ushindi huo wa Bayern wa 19 mfululizo Bundesliga uliwahakikishia taji lao la 24 – lao la 23 enzi ya Bundesliga – na ushindi huo katika uwanja wa Olimpiki wa Berlin haukiwa wa kutiliwa shaka kwani walikuwa wamepata uongozi wa 2-0 baada ya dakika 15 za uchezaji.
Bayern pia wameondoa mechi moja kutoka kwenye rekodi yao waliyoweka msimu uliopita, kwa kushinda ligi mapema zaidi, nab ado wamo mbioni kumaliza ligi wakiwa hawajashindwa.
“Ni jambo la kusisimua sana kushinda taji ukiwa pia na rekodi ya kutoshindwa,” alisema winga Arjen Robben.
"Tunajionea fahari sana kwa timu yetu na ufanisi wetu msimu huu.”
Kiungo wa kati Toni Kroos alifunga bao la mapema kabla ya Mario Goetze kufunga la pili kwa kichwa na kusaidia miamba hao wa Bavaria kujihakikishia alama tatu walizohitaji kutwaa taji usiku huo.
Straika wa Hertha kutoka Colombia Adrian Ramos alifunga penalti kabla ya winga wa Ufaransa Franck Ribery kutoka benchi na kufunga la tatu.
Wakiwa na mechi saba zilizosalia, haiwezekani sasa kwa Bayern kufikiwa na wapinzani wao, ingawa kwa kweli mbio za kushinda ligi zilikuwa zimeamuliwa mapema.
"Kila kitu kimetufaa wakati huu. Tumecheza soka vyema sana msimu huu,” alisema kipa wa Bayern na Ujerumani Manuel Neuer.
"Tuna furaha sana kuwa na Pep Guardiola hapa. Ameimarisha uchezaji wetu zaidi.”
Kroos, ambaye mashauriano yake ya majuzi ya kuongeza mkataba wake yamekwama, alianza ufungaji mabao dakika ya sita alipofunga kutoka wka krosi ya Mueller.
Goetze alifunga la pili kwa kichwa kutoka kwa mpira wa Bastian Schweinsteiger dakika nane baadaye na Bayern walijivunia udhibiti wa asilimia 83 wa mpira kipindi cha kwanza.
Mambo yangekuwa 3-0 wakati wa mapumziko baada ya Mueller kugonga mpira wa kichwa lakini ukatoka nje baada ya kugonga mwamba wa goli baada ya kumbwaga kipa wa zamani wa Bayern Thomas Kraft ambaye sasa hushikia Hertha dakika saba kabla ya muda wa mapumziko.
Wenyeji walikomboa moja baada ya Ramos kufunga penalty baada ya kufanyiwa madhambi eneo la hatari dakika ya 66 na beki wa kulia wa Brazil Rafinha.
Hata hivyo, dakika 11 kabla ya mechi kuisha, Ribery alifunga bao bora la usiku huo baada ya kufunga kutoka kwa pembekali baada ya Goetze kukimbia na mpira kwa ustadi.