come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

ATLETICO MADRID YAPEWA NAFASI KUBWA KUILAZA REAL MADRID

Koke

Atletico Madrid wana nafasi murwa Jumamosi kusherehekea taji lao kuu la kwanza barani Uropa kwa kuwazuia majirani wao asimu na wakwasi amiza ya kuandikisha historia kwa kushinda taji lao la 10 la ligi ya mabingwa.

Atletico wamejizatiti pakubwa tayari musimu huu kwa kunyakua ligi ya Uhispania, La Liga na kukomesha utawala wa miamba Barcelona na watanashari wao Real kwa mara ya kwanza tangu Valencia walivyofanikiwa kuvunja mtindo huo 2004.

Vijana wa Diego Simeone wamerejea kwenye meza kuu ya Uropa baada ya kungonjea kuwania fainali hiyo kwa mara ya kwanza tangu 1974 waliposalimu amri mikononi mwa Bayern Munich.

Isitoshe, hiyo itakuwa mechi ya kwanza ya maamuzi kushirikisha vilabu jirani katika historia ya miaka 59 ya shindano hilo.


Real wanatambulika kama klabu tajiri zaidi duniani kwa mapato na wametumia kitita kikuu cha zaidi ya Euro milioni 600 kununua wachezaji wa fahari miaka mitano iliyopita katika juhudi ya kutwaa taji al maarufu ‘La Decima’ Uhispania au ushindi wa 10 wa taji hilo kuu.

Rais wa Real, Fiorentino Perez hajasita kumimina noti ili kupata huduma za viungo matata duniani wakiongozwa naye mchezaji bora zaidi duniani, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale aliyegharimu kiasi kikubwa duniani kinachokisiwa kuwa Dola milioni 100.

“Kutoka siku ya kwanza mchezaji anapoingia klabu hiki, tayari anasema amekuja kushinda Decima,” mshambuliaji wa zamani wa Real, Predrag Mijatovic aliambia gazeti la Uhispania la Marca.
“Hilo ni shinikizo kubwa sana kwa wachezaji,” straika aliyefunga bao la ushindi walipowapiku Juventus 1-0 katika fainali ya kombe hilo ya 1998 aliongeza.

Atletico, wanaofahamika kama ‘watengenezaji ya migodoro’ kwa sababu ya sare zao zenye msitari mieupe na nyekundu watapambana na Real mashuhuri kama “meringues” kwa sababu ya kucheza na nguo nyeupe.
Itakuwa mara ya pili ya waasimu hawa kutoana jasho ulingoni huo tangu musimu wa 1958-59 walipochuana katika semifainali iliyoshudia Real wakitamba hadi fainali kwa kushinda mechi ya marudiano 2-1.