come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

SCHOLES AANZA KUMTISHA VAN GAAL

Paul Scholes

Kiungo aliyestaafu mashuhuri cha Manchester United, Paul Scholes, amesema meneja mpya wa miamba hao wa Uingereza, Luis Van Gaal, anakibarua ‘kigumu zaidi’ mikononi mwake kufufua hadhi ya timu hiyo.

Scholes aliendelea kuuliza ikiwa wasimamizi wakuu wa timu hiyo wana nia na ari ya kurejesha mabingwa hao walingatuliwa musimu huu hadi kilele kama ilivyo kuwa itikadi yao hadi kampeni iliyoisha juzi.

Alizidi kunena kuwa kiungo cha kati wa Bayern Munich, Toni Kroos, ndiye anayefaa kusainiwa na van Gaal kwanza katika harakati za kujenga upya kikosi cha washindi hao mara 20 wa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza walioshuka hadi nafasi ya saba musimu huu.
“Ametumikia vilabu kubwa duniani lakini ana kazi ya ziada hapa Man United mikononi mwake.


“Itakuwa pengo kubwa kujaza ili kushika Manchester City, Chelsea na Liverpool musumu ujao. United wako nyuma sana. Van Gaal akiwaongoza kufuzu ligi ya mabingwa itakuwa ni mwanzo,” alisema Scholes.

Naibu mwenyekiti mtenda kazi, Ed Woodward, alikuwa mshawishi mkuu kumleta van Gaal kufuatia kufutwa kwa David Moyes kama meneja lakini Scholes aliongeza hata yeye ana jukumu la kujidhihirisha kwenye musimu huu wa kiangazi.

“Kazi ni kwake kuonyesha ana uwezo wa kushawishi wachezaji wakuu wajiunge na timu hii ikiwa ana weledi wa kazi yake,” kiungo huyo aliyestaafu misimu miwili iliyopita baada ya kutumikia na kushinda mataji kocho kocho na timu hiyo alisema.