come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

NIKI WA PILI ASUSA KUTOA ALBUM

Na Robert Michael

Msanii wa music wa Hiphop "Niki wa pili" (Pichani) akireport katika hii blog amesema kuwa pamoja na tasnia ya music wa Hiphop kuizalishia serikari kiasi cha shilingi "Milioni 40" ameshindwa kuuza "Album" kutokana na udogo wa maslai.


Aidha msanii huyo ambae anafanya vizuri katika kundi lake la "Weusi" amesema anashiriki vizuri katika kundi hilo na kipato chao asilimia kubwa wanawekeza kwenye ubunifu na hawashindwi kubadilisha "Style na beat".

Niki wa pili ameona ni bora kuuza single kuliko kuuza Album akidai kuwa lengo la kazi yake afanye Music apate pesa kama hakuna pesa hawezi fanya "Music".

Ameona kuwa endapo Music utakuwa haulipi atafanya mambo mengine ya kibiashara.

Msanii huyo anaetamba na wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni unaoitwa "Sitaki kazi" amesema ukosefu wa Ajira ni tatizo nchini Tanzania.

Pia amewataka vijana wanaosoma, wasome na kufikiria namna ya kupata Ajira kwani music haulipi kama anavyofikiria yeye.