come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

ALIYEMROGA CRISTIANO RONALDO BALAA, AUMIA TENA GOTI SASA HOFU TUPU KIKOSI CHA URENO

MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo ameba hofu upya ndani ya kikosi cha Ureno kuelekea mchezo wao wa ufunguzi wa Kombe la Dunia dhidi ya Ujerumani baada ya leo kutoka uwanjani mazoezini akiwa amefungwa barafu kwenye goti.


Nyota huyo wa Real Madrid alipata ahueni wiki hii na kuanza mazoezi hivyo kurejesha amani Ureno, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ameibua hofu upya juu ya hali yake.

Ronaldo alimudu kufanya mazoezi kwa dakika zisizozidi na wachezaji wenzake kabla ya kulazimika kutoka.