
Meneja wa Manchester City, Manuel Pellegrini amekataa kuzungumza na Chama cha Soka cha Brazil kuhusu kuchukua nafasi ya Luiz Filipe Scolari kuifundisha timu ya taifa (El Mercurio).

Swansea wamekataa pauni milioni 8 zilizotolewa na Liverpool kumsajili Ben Davis (Daily Telegraph), Manchester United, Chelsea na Arsenal watatakiwa kutoa zaidi ya euro milioni 75 ili kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain, Edison Cavani (talkSPORT)
Everton wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Fevencvaros Muhamed Besic kwa pauni milioni 4 (Daily Mail), Trabzonspor ya Uturuki wanamfuatilia beki wa Liverpool Kolo Toute (Daily Mail)

Besitkas wanamtaka Demba Ba, 29, kwa mkopo huku wakitaka kufanya uhamisho huo kuwa wa kudumu baada ya msimu (Daily Mirror), AC Milan wanamtaka winga wa Manchester United Nani (Football Italia)
Manchester United wanawafuatilia kwa makini kuwapa majaribio Joao Virginia, 15, aliyepewa jina la 'Cristiano Ronaldo mpya' na kipa Joao Virginia, 15, kutoka Porto (Skysports)