Mpaka siku ya mwisho ya kupeleka
maombi ya kuandaa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2017 ni mataifa
saba tu yaliyotuma maombi kuandaa michuano hiyo,hapo jana ililipotiwa ya kwamba
Tanzania imetolewa kwenye mchakato huo wa maombi baada ya kuambiwa na CAF kuwa
haina uwezo wa kuandaa hayo mashindano kwasasa,
Taarifa ambazo mtandao huu umezipata kutoka Makao makuu ya CAF jijini Cairo zinasema Tanzania haikupeleka maombi ya kuandaa mashindano hayo yanayotarajia kufanyika mwaka 2017.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya CAF
mataifa yaliyotuma maombi rasmi kabla ya muda kufungwa hapo mnamo septemba
30,2014 ni Algeria, Egypt, Gabon, Ghana, Kenya, Sudan na Zimbabwe.
Maombi
ya kuandaa mashindano hayo yalifunguliwa rasmi 23 August 2014, kufuatiwa
kujiondoa kwa Libya,
Mwandaaji atakayepata nafasi atatangazwa na kamati ya utendaji ya CAF kupitia moja ya vikao vyake mnamo mwaka 2015.
Mwandaaji atakayepata nafasi atatangazwa na kamati ya utendaji ya CAF kupitia moja ya vikao vyake mnamo mwaka 2015.