come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

SUAREZ AANZA KUSAKA BAO LAKE LA KWANZA AJAX

Luis Suarez 

Straika matata wa Barcelona, Luis Suarez, atarudi uwanja safari yake ya kutafuta maarufu Ulaya ilianza wakati miamba hao wa Uhispania watakapoalika timu yake ya zamani Ajax Amsterdam ya Uholanzi Jumatano akiwa na lengo moja pekee.

Imekuwa ni mechi mbili sasa na klabu chake kipya baada ya kutumikia maarufu ya miezi mine kutoka kandanda bila ya kubusu wavu lakini ngoma dhidi ya Ajax inampatia raia huyo wa Uruguay fursa safi ya kukata kiu chake cha mabao.

Suarez alifungia Ajax mabao 111 kwenye kikao chake cha miaka mine kama mchezaji wa mabingwa hao wa Uholanzi kabla ya kuhamia Liverpool wa Uingereza mwakani 2011 lakini bado hajafanikiwa kutia kizimbani tangu asaini na Barcelona kwa kitita kimono cha pauni milioni 75 musimu wa kiangazi uliopita.


Washambuliaji wazito wa Barca, Suarez, Neymar na Lionel Messi walitumbukia nyongo wikendi iliyopita walipokumbana na jabali kwenye goli la Celta Vigo, Sergio Alvarez, pamoja na mkosi wa kugonga ulingo wa lango mara nne katika ngoma ya La Liga Jumamosi iliyopita waliposalimu amri kwa mshtuko 1-0.
Kulazwa huko kulifuata fedheha ya kukomolewa 3-1 na watanashari wao Real Madrid katika kivumbi cha El Clasico juma lililotangulia huku matokeo hayo yakiwafanya washuke hadi nafasi ya tatu katika jadwali la La Liga.

“Mechi dhidi ya Ajax ndiyo muhimu kwangu kwa sasa. Ni klabu ambacho kilinipa kila kitu ila nifanikiwe. Nilijifunza mengi na nitawashukuru milele. Kurudi kucheza Ligi ya Mabingwa na Barcelona ni jambo kuu kwangu,” Suarez alisema.

Ikiwa Barcelona watafanikiwa kutamba kuambatana na wapinzani wao Paris St Germain kushinda nyumbani dhidi ya APOEL Nicosia, basi vigogo hao wawili watajikatia tiketi zao za awamu ya 16-bora kutoka Kundi F mechi mbili zikisalia.

Barca wanachukua tahadhari kubwa dhidi ya Ajax kwani ndio walikuwa wa kwanza kuwalaza musimu huu walipowanyoa 2-1 jijini Amsterdam majuma mawili yaliopita.