come
KIUNGO AZAM FC ATAKIWA SLOVENIA
KLABU ya Maribor FC ya Slovenia inamtaka winga kinda wa Azam FC, Farid Mussa Malik (pichani kulia) na tayari ipo katika mawasiliano na klabu yake.
Maribor, moja ya klabu kongwe nchini Slovenia na ambayo haijawahi kushuka Ligi Kuu tangu ilipoanzishwa mwaka 1991, imevutiwa na Farid baada ya kupata video zake kupitia kwa wakala wake.
Lakini pia ilimfuatilia yenyewe kwenye baadhi ya mechi akiichezea timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ na kujiridhisha ni mchezaji mzuri na sasa inajaribu kumhamishia Ulaya.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba hakupatikana tangu jana alipotafutwa kuzungumzia suala hilo.
Farid aliyepandishwa kutoka akademi ya Azam FC, ametokea kuzivutia klabu nyingi ndani ya nje ya nchi na kumekuwa na tetesi pia, TP Mazembe nayo inamtaka.
Hata hivyo, inaonekana Azam FC haitakuwa tayari kumuachia kwa urahisi kinda huyo – labda litolewe dau kubwa la uhamisho.