Timu ya Arsene Wenger, Arsenal imetinga
Ligi ya Mabingwa kwa mara ya 16 na kujipatia kitita cha Pauni
zisizopungua Milioni 25, baada ya kuifunga Newcastle 1-0 bao pekee la
Laurent Koscielny dakika ya 51 Uwanja wa St James Park. Sunderland nayo ilishinda 1-0, dhidi ya Sunderland bao pekee la Gareth Bale dakika ya 89.
Chelsea
imemaliza katika nafasi ya tatu kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Everton,
mabao yake yakitiwa kimiani na Mata dakika ya sita na Torres dakika ya
75, huku la wapinzani wao likifungwa na Naismith dakika ya 13 Uwanja wa
Stamford Bridge.
Katika
mechi nyingine, mabingwa Manchester United wametoka sare ya 5-5 na West
Brom, Uwanja wa The Hawthorns. Mabao ya United yalifungwa na Kagawa
dakika ya tano, Olsson aliyejifunga dakika ya nane, Buttner dakika ya
29, Van Persie dakika ya 52 na Hernandez Chicharito dakika ya 62, wakati
wa WBA yalifungwa na Morrison dakika ya 39, Lukaku dakika ya 49, 80 na
85 na Mulumbu dakika ya 80.
Liverpool imeshinda 1 - 0 dhidi ya QPR, bao pekee la Coutinho dakika ya 22 Uwanja wa Anfield, Manchester City imechapwa 3-2
nyumbani na Norwich. Mabao ya City yalifungwa na Rodwell dakika ya 28
na 58 na ya wapinzani wao yalifungwa na Pilkington dakika ya 25, Holt
dakika ya 53 na Howson dakika ya 64.
Southampton imetoka
1 - 1 na Stoke, West Ham imeichapa 4 - 2 Reading, Swansea imefungwa
3-0 nyumbani na Fulham wakati Wigan imetoka 2 - 2 na Aston Villa
nyumbani pia
Bale akishangilia bao lake linaloiwezesha Spurs kucheza Europa League msimu ujao
Mamilioni ya Euro: Beki wa Arsenal, Laurent Koscielny akiifungia timu yake bao pekee Uwanja wa St James Park
Akipongezwa na wachezaji wenzake wa Arsenal, Aaron Ramsey, Santi Cazorla na Bacary Sagna
Cazorla akiwapongeza wenzake