London, England. Rio Ferdinand anatarajia kusaini mkataba mpya
na Manchester United wakati wowote kuanzia sasa, taarifa za ndani za
klabu hiyo zilithibitisha jana.
Kocha mpya, David Moyes anatarajiwa kumpa mkataba
wa mwaka mmoja baada ya ule wa kwanza kumalizika mwezi ujao. Tayari beki
huyo ameshatangaza kuachana na soka la kimataifa ili aendelee kucheza
Old Trafford.
Ferdinand amecheza mechi 33 msimu huu, zikiwemo 27
za Ligi Kuu ambazo ni nyingi kuliko beki mwingine yeyote wa nafasi ya
kati na kuiwezesha Man United kutwaa ubingwa msimu huu. (BBC).