Mume wa Malkia wa Mipasho Khadija Koppa ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mogomeni Bagamoyo kupitia CCM Jaffar Ali Yusuf amefariki dunia mapema asubuhi ya leo katika Hospitali ya lugalo. Kwa mujibu wa baadhi ya ndugu wa marehemu wamesema kuwa ndugu yao alikuwa anasumbuliwa na
tatizo la mfumo wa upumuaji.
Wadau wa tasnia ya taarabu nchini wametoa salamu zao za pole kwa malkia wa mipasho nchini Bi Hadija Omari Kopa kufuatia msiba huo wa kuondokewa na mumewe, Majuto Mbiligenda mkurugenzi wa gazeti la Kabumbu ameonyesha masikitiko yake kufuatia msiba huo mkubwa