Boban alisaini mkataba wa kujiunga na Coastal
Jumapili ya wiki iliyopita baada ya uongozi wa klabu ya Simba
kutoonyesha nia ya kumuhitaji tena.
Awali uongozi wa Simba ulimsimamisha Boban na
wachezaji wengine saba wa timu hiyo baada ya kuwashutumu kuwa ni watovu
wa ndhamu. Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu jana,
Circkovic alisema kuwa uamuzi wa Boban ni sahihi kwani utamwezesha
kulinda kipaji chake kwani kilikuwa mbioni kupotea.
“Nimesikia Boban amehamia Coastal Union, ni uamuzi sahihi kabisa,”alisema kocha Circkovic.
Alisema,”Kama Simba wameonyesha hawamuhitaji ni
bora ameondoka mapema kwa sababu hata kama atabaki hataweza kucheza
hivyo itakuwa hasara kwa kipaji chake,” alisema Cirkovic.
Alisema anaamini tatizo linaloikabili Simba wakati
huu ni chuki binafsi za baadhi ya viongozi wa Simba na siyo utovu wa
nidhamu wa wachezaji.
Kocha Cirkovic aliwatahadharisha viongozi wa Simba
kama wasipobadilika timu yao haitapata mafanikio. Pia, Cirkovic
alipinga kitendo kilichofanywa na uongozi wa Simba cha kusitisha mkataba
wa kocha wa timu hiyo Patrick Liewig, akisema siyo suluhu ya kusaka
mafanikio.