Congo, Ivory Coast na
Tunisia zimepiga hatua kubwa kuelekea Kombe la Dunia baada ya kushinda
mechi zao za Jumamosi japokuwa ushindi huo ulifunikwa na kasi ya
Ethiopia.
Ethiopia ilishinda 2-1 dhidi ya Botswana na
kujiweka katika nafasi ya kufuzu kwa hatua ya mtoano kama watashinda
mechi yao ya wiki ijayo.
Mabao mawili katika kipindi cha kwanza
yaliyofungwa na Getaneh Kebede na Saladin Seid ambaye ni bao lake la
nne, yalitosha kuiweka Ethiopia kileleni mwa Kundi A ikiwa na pointi 10
katika mechi nne ilizocheza.
Wapo mbele kwa pointi mbili kwa wenyeji wa Kombe la Dunia 2010, Afrika Kusini ambao ni wapinzani wao wajao.
Ethiopia ilifuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika
2013 baada ya kuwa nje kwa zaidi ya miaka 30, na walithibisha ubora wao
katika fainali hizo.
Afrika Kusini ilishinda 3-0 dhidi ya Jamhuri
Afrika Kati na kufuzu matumaini yao katika mchezo huo uliochezwa kwenye
uwanja huru nchini Cameroon kwa sababu ya mapinduzi ya Serikali ya
Bangui.
Congo na Tunisia walipoteza rekodi yao ya asilimia 100, lakini walifanikiwa kupata sare na kujiweka vizuri katika makundi yao.
Beki Christopher Samba alishuhudia mchezo huo
wakati Congo wakilazimishwa suruhu na majirani zao Gabon mchezo
uliofanyika Franceville na kufikisha pointi sita katika Kundi E.
Bao la dakika za mwishoni la Fakhreddine Ben
Youssef ilitosha kuipa Tunisia sare 2-2 na dhidi ya Sierra Leone na
kuwafanya kuwa mbele kwa pointi tano katika Kundi B.
Tunisia watajihakikisha kufuzu kama watafanikiwa kuifunga Equatorial Guinea wiki ijayo.
BAO LA TOURE
Mwanasoka bora wa mwaka Afrika, Yaya Toure alikuwa
miongoni mwa wachezaji waliofunga mabao ya Ivory Coast walipoichakaza
Gambia kwa mabao 3-0 na kuongoza Kundi C kwa pointi 10.