BONDIA Mada Maugo maarufu kama ‘King Junior’, juzi amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Bondia huyo ambaye anapigana uzito wa kati,
alikabidhiwa kadi jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Chadema, Wakili Mabere Marando kwenye sherehe za kuchangia kampeni za
udiwani Kata ya mianzini. Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhiwa
kadi hiyo Maugo alisema ameamua kujiunga na Chadema baada ya kuvutiwa na
sera za chama hicho na kwamba siyo mambo mengine.
“Mimi ni kijana mpenda maendeleo, leo nimeamua
kujiunga na Chadema kwa ridhaa yangu mwenyewe baada ya kuvutiwa na sera
za chama hiki,” alisema Maugo.
Alisema, “Kupitia uwepo wangu ndani ya Chadema
nitatumia nafasi hii vizuri kwa kushirikina na vijana wengine ili
kuhakikisha tunatafuta maendeleo na ukombozi wa nchi yetu.”