Diamond ataongeza listi ya burudani mara baada ya
mabondia kutoka Kenya, Patrick Amote na Shadrack Machanje kuvaana na
Watanzania, Thomas Mashali na Francis Miyeyusho kuzichapa ndani ya
Uwanja wa Taifa, Julai 7, mwaka huu ndipo mkali huyo atakaposhusha zile
ngoma kali zenye meseji nzuri za mapenzi.
Mratibu wa tamasha hilo, Abdallah Mrisho ‘Abby
Cool’ amesema listi ya wasanii wa Bongo Fleva watakaopafomu siku hiyo
itazidi kuongezeka kadiri siku zinavyozidi kuyoyoma na burudani kabambe
inatarajiwa kuwekwa na timu za mpira wa miguu kati ya Bongo Movies na
Bongo Fleva.
“Matukio makubwa yatatokea, Diamond atamaliza
kupiga nyimbo zote kali. Tutakuwa na wasanii wengine kibao kutoka ndani
na nje ya Bongo, mashabiki waanze kujipanga kwa ajili ya kuiandika
historia,” alisema Abby Cool.
Mwenyekiti wa Bongo Movie, Vincent Kigosi ameahidi
timu yake ipo fiti na wataibuka na ushindi huku Hamisi Ramadhan ‘H.
Baba’ kiongozi wa Bongo Fleva akidai wao ndiyo wababe.
Mbali na burudani hiyo ya muziki na mechi ya
mipira wa miguu, kutakuwa na mpambano wa ndondi za utangulizi kati ya
Ramadhani Mkundi na Martin Richard.
Ili kushuhudia matukio hayo ya kihistoria,
mashabiki watazama uwanjani kwa kiingilio cha shilingi 20,000 V.I.P,
viti vya bluu 10,000 na 5,000 viti vya kawaida.