come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

Historia ya kiburudani kuandikwa leo!


Siku iliyosubiriwa kwa hamu na wadau wa muziki nchini ya tamasha la miaka 13 katoka kwa mwamuziki Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee na The Finest ya mwanamuziki Khamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ imetimia leo
.

The Finest ya Mwana FA itafanyika pale Makumbusho jirani na chuo cha IFM, huku miaka 13 katika muziki ya Jaydee inatarajiwa kufanyika Nyumbani Lounge.
Baada ya kuahirishwa Mei 31 shoo hizi mbili zote kwa pamoja zinatarajiwa kufanyika leo Juni 14 katika maeneo mawili tofauti hali inayoendelea kuwachanganya mashabiki wengi nani alitangulia kutangaza tarehe awali.
Mei 29 baada ya kifo cha marehemu Albert Mangwea, Mwana FA aliandika twitter “Sina uhakika, lakini nimeahirisha shoo yangu mpaka June 14 kama kaka tutakuwa tumeshampumzisha,” alitweet FA.
Lakini Jaydee aliahirisha na kusema atatangaza ni lini shoo yake itafanyika, baadaye alikuja kuandika twitter “Ni wiki ndefu kwangu Juni 13 mahakamani, Juni 14 Miaka 13 ya Jide. Juni 15 ni siku yangu ya kuzaliwa, ni Juni ni mwezi wangu,” alitweet Jide.
Mwanamuziki FA amesema asilimia 15 ya mapato kutoka katika shoo hiyo, yatapelekwa kwa mama mzazi wa Ngwea.
“Nimesema nitoe hela mfukoni kwangu moja kwa moja, niipeleke huku, kwa hiyo chochote nitakacho kipata, nataka kutoa asilimia 15