MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesema kwamba anajuta kusaini Mkataba wa muda mrefu Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kwani kwa sasa unaonekana kumbana kusogea mbele kwenye maslahi zaidi.
Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam, Samatta alisema kwamba kuna klabu
nyingine ambazo zinaweza kumlipa vizuri kuliko anavyolipwa Mazembe,
lakini zinaogopa hata kuifuata timu hiyo ya DRC kutokana na sera yake
ngumu ya kuuza wachezaji.
“Kwa mfano Orlando Pirates, walionyesha nia ya kunitaka, ila wakaogopa hata kuwafuata Mazembe, kwa sababu wanajua ni vigumu kuchukua mchezaji Mazembe. Kwa hiyo sina jinsi, inabidi nisubiri hadi wenyewe (Mazembe) wakiwa tayari kuniuza, au hadi nimalize Mkataba,” alisema.
Samatta alisema anafurahia maisha Lubumbashi, analipwa vizuri na anahudumiwa vizuri, ikiwa ni pamoja na kukubalika mbele ya mashabiki, lakini pamoja na yote bado anataka kusogea mbele kukabiliana na changamoto mpya.
“Kiu yangu haswa ni kucheza Ulaya, kipindi hiki cha majira ya joto ndiyo klabu zinasaka wachezaji, kwa kweli naomba sana Mungu anijaalie nipate nafasi ya kusogea Ulaya, hiyo haswa ndiyo kiu yangu,”alisema Samatta.
Alipoulizwa sababu za kusaini Mkataba mrefu na Mazembe, Samatta alisema; “Wakati ule mimi fikra zangu zilikuwa ni kutoka kwanza hapa nyumbani, kupata maslahi makubwa zaidi ya niliyokuwa Napata nyumbani. Na ni fedha nyingi, tena sana, ambazo sidhani kama kuna klabu nyingine yoyote inaweza kunipa nyumbani,”.
“Sema kadiri mtu unavyosogea mbele, ndivyo unavyozidi kupata matamanio zaidi ya kufika mbali zaidi. Inaniuma sana nikisoma kwenye magazeti na mitandao, mtu fulani analipwa fedha kiasi fulani Ulaya, wakati nikiangalia mimi nina uwezo kuliko yeye,”alisema.
Samatta alisajiliwa na Mazembe kwa mkataba wa miaka mitano kutoka Simba SC miaka miwili iliyopita kwa dau la rekodi kwa mchezaji wa Tanzania kuuzwa nje, dola za Kimarekani 150,000 (zaidi ya Sh. Milioni 200).
Simba SC ilivuna mamilioni ya kumuuza nyota huyo miezi kadhaa tu tangu imnunue kwa bei chee (haikufka hata Sh. Milioni 10) kutoka African Lyon ya Dar es Salaam.
Hata hivyo, kuna uwezekano Samatta katika majira haya ya joto akahamia Ulaya, kwani mawakala wengi wamekuwa wakimfuatilia naye ameendelea kufanya vizuri.