come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

RASHID MATUMLA AMTAMANI CHEKA

BONDIA mkongwe wa ngumi za kulipwa nchini Rashid Matumla 'Snake Man' ambaye alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kupooza miguu kwa muda mrefu sasa amepona tatizo lake na yuko fiti kwa pambano.


Akizungumza leo na mtandao huu amesema kuwa kwa sasa amepona na yuko tayari kupanda ulingoni kuzipiga na bondia yeyote yule, Matumla amedai kuwa kiwango chake bado hakijashuka na anayetaka kupoima uwezo wake akubali kuzichapa naye.

Matumla ambaye alipata kuwa bingwa wa dunia uzito wa Super Walter unaotambuliwa na WBU alijikuta anapoteza hadhi yake baada ya kuchapwa mfululizo na bondia anayekuja juu kwa sasa nchini Francis Cheka wa Morogoro.

Lakini katika maelezo yake, Matumla amesema kuwa alikua akipigwa na Cheka kutokana na klusumbuliwa na maradhi ya miguu ila kwa sasa yuko fiti baada ya kupatiwa matibabu.

Pia Matumla amemsifu rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe Jakaya Mrisho Kikwete kuwa ndiye aliyemtafutia daktari hadi amepona matatizo ya mguu.

'Kusema kweli nilikuwa siwezi hata kusimama, Lakini niliamua kuwasiliana na mheshimiwa Kikwete ambapo hakusita na alinitafutia daktari hatim aye nimepona tatizo langu, Lakini hata hivyo wakati nikiumwa niliiwambia mabondia ninaopigana nao kuwa hamuwezi kunipiga katika raundi za mwanzo labda kwa pointi', alisema na kuongeza.

'Katika michezo yangu niliyopigwa nilipigwa kwa pointi tena kwa mbinde sana, Lakini sasa niko fiti na nipo tayari kuzip[iga na bondia yeyote yule hata Cheka', alisema.