come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

Redds Miss Tanga kutwaa 500,000/-

Mkurugenzi wa Kampuni ya DATK Entertainment, Asha Kigundula
Mrembo atakayeshinda taji la urembo mkoa wa Tanga "Redd’s Miss Tanga 2013' litakalofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkwakwani atapata zawadi ya Sh. 500,000.


Mkurugenzi wa Kampuni ya DATK Entertainment inayoandaa shindano hilo, Asha Kigundula, alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yamekamilika na mshindi wa pili atajinyakulia Sh. 300,000, mshindi wa tatu Sh. 250, 000 wakati mshindi wa nne na tano kila mmoja ataondoka na Sh. 200,000.

Alisema kuwa warembo wengine watakaobaki, kila mmoja atapata kifuta jasho cha Sh.100,000 na pia kutakuwa na zawadi nyingine kwa mrembo mwenye nidhamu itakayotangazwa jukwaani siku ya shindano hilo.

Alisema kutakuwa pia na zawadi kwa washindi watatu watakaofanya vizuri katika shindano la vipaji (talent), ambapo mshindi wa kwanza atajinyakuliwa Sh.100,000 na mshindi wa pili na watatu kila mmoja atapewa Sh.50,000.

Alimtaja msanii wa kizazi kipya, Tunda Man, ataongoza safu ya burudani pamoja na Dr John, Nabisha kutoka kundi la THT, Fady Dady na wasanii chipukizi kutoka mkoani Tanga.

Alisema shindano hilo litaanza saa 2:00 usiku na warembo 12 watapanda jukwaani kuwania taji hilo.

Warembo hao ni Hawa Ramadhani (18), Hazina Mbaga (19), Like Abdulraman (19), Irene Thomas (20), Tatu Athumani (19), Winfrida Gutram (21), Lulu Mbonela (19), Hazina Daniel (19), Lulu Matawalo(22), Judith Mollel (21), Neema Jonas na Hawa Twaybu (21).

Wakati huo huo, warembo hao wanaowania taji la mkoa wa Tanga wameiomba Halmashuri ya Jiji la Tanga kuifanyia marekebisho barabara inayokwenda katika mapango ya Amboni ili ipitike kirahisi nyakati zote.

Ombi hilo lilitolewa na warembo hao mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea mapango hayo ambapo walikwenda kujifunza historia yake pamoja na kuingia mapangoni, lengo likiwa ni kujifunza utalii wa ndani ili kuutangaza kwa wageni na jamii nzima.