come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

ROONEY KUTUA REAL MADRID, MAN UNITED IKIJICHANGANYA IMEKULA KWAO

Highly rated: But Wayne Rooney's future remains uncertain
KOCHA mpya wa Real Madrid, Carlo Ancelotti atafanya harakati za kumsajili Wayne Rooney majira haya ya joto kama mshambuliaji huyo asiye na furaha atashindwa kumaliza tofauti zake na Manchester United.
inafahamika kuwa Rooney anapenda zaidi kuungana na Jose Mourinho pale Chelsea ikiwa atamaliza miaka yake tisa ya kuishi United, lakini Madrid itakuwa na nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ikiwa ataondoka.
Matawi ya juu: Lakini mustakabali wa Wayne Rooney bado upo shakani.

Klabu zote zina uwezo sana tu wa kulipa Pauni Milioni 30 za ada ya uhamisho wake na kumlipa mchezaji mwenyewe mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki.
Kocha wa zamani wa Chelsea, Ancelotti anatarajiwa kuthibitishwa kuwa mrithi wa Mourinho Jumatatu na atakabidhiwa orodha ya wachezaji wanaotakiwa, wakiwemo Rooney, Gareth Bale, Edinson Cavani na Luis Suarez.
Rooney, ambaye amebakiza miaka miwili katika Mkataba wake, atakuwa na mazungumzo na kocha mpya wa United, David Moyes baada ya wote kurejea kutoka mapumzikoni siku chache zijazo, lakini inaonekana kama atabadilisha mawazo yake juu ya kwenda kuanza maisha mapya.
Ambitious: Carlo Ancelotti would like Rooney to follow him to Real Madrid
Matarajio: Carlo Ancelotti angependa Rooney amfuate yeye Real Madrid

Wakati huo huo, kocha wa zamani wa Ufaransa, Laurent Blanc anajiandaa kurithi mikoba ya Ancelotti ya ukocha wa Paris Saint-Germain.
Baada ya mpango wa mabingwa hao wa Ufaransa kumchukua kocha wa zamani wa England, Fabio Capello kukwama, sasa beki wa zamani wa Manchester United, Blanc, mwenye umri wa miaka 47 atapewa mikoba.  
Laurent Blanc
Fabio Capello
Uteuzi: Laurent Blanc atarithi  mikoba ya Ancelotti PSG baada ya kukosekana Fabio Capello 

"Makubaliano yamefikiwa leo kati ya Paris St Germain na Laurent Blanc, kwa yeye kuwa kocha mpya wa klabu ya Jiji," taarifa ilisema.
"Makubaliano baina ya kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa na PSG yamekubaliwa kwa miaka miwili. Ilipangwa kwamba, atasaini Mkataba wiki ijayo,".