SIMBA na Yanga
hazitashiriki michuano ya Kombe la Kagame nchini Sudan, iwapo Serikali
itasisitiza amani iliyopo nchini humo siyo salama, Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) lilisema jana Dar es Salaam.
Kabla hata TFF haijatoa kauli hiyo kupitia kwa
Mtendaji Mkuu, Angetile Osiah, Serikali ilishatoa angalizo juu ya utata
wa usalama nchini Sudan hasa kwenye Mji wa Darfur ambako ni sehemu ya
kituo cha michuano hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe alisema bungeni wiki iliyopita wakati wa
mjumuisho wa hotuba yake kuwa, Serikali haitakuwa tayari kuziruhusu timu
zake kwenda kushiriki mashindano hayo.
Jana, Osiah alisema TFF itatekeleza agizo la
Serikali kuhusu hali ya usalama, na kwamba Simba na Yanga ambao ni
mabingwa wa taji hilo hazitakwenda Sudan kinyume na agizo la Serikali.
“Kauli ya Membe ni muhimu. Serikali imejali
usalama wa watu wake,” alisema Osiah. “Tunaendelea kuwasiliana na
Serikali kupitia ubalozi wetu Sudan kabla ya kutoa msimamo kutegemeana
na tutakavyoelezwa. Kuna taarifa timu ya El-Merrheikh na Al-Hilal
zimejitoa katika mashindano hayo kwa hofu ya usalama nchini humo.