MBWANA Samata na Thomas Ulimwengu wametuma salamu Morocco baada
ya kuiongoza TP Mazembe kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la
Shirikisho.
TP Mazembe ilipokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Liga Muculmana ya Msumbiji, lakini wamesonga mbele kwa ushindi wa jumla 5-2.
Mshambuliaji Samata alifunga bao la kufutia machozi la Mazembe akiunganisha kwa kichwa kona ya Solomon Asante.
Hilo ni bao la tatu kwa Samata kufunga katika wiki
moja baada ya kupachika mabao mawili waliposhinda 5-0 katika mechi ya
Ligi Kuu DR Congo dhidi ya Molunge.
Katika mchezo huo wa ligi uliofanyika Kinshasa
Jumanne iliyopita, Samata alifunga mabao mawili huku Ulimwengu na Given
Singuluma, na Eric Bokanga kila mmoja akifunga bao moja.
Kasi ya Samata na Ulimwengu ilitosha kuisaidia
Taifa Stars kuisambaratisha Morocco katika mchezo wa kusaka kufuzu
kushiriki Kombe la Dunia 2014 uliofanyika mwezi Machi 24, ambapo Taifa
Stars ilishinda kwa mabao 3-1.
Nyota hao wa TP Mazembe watajiunga na kambi ya
Stars nchini Morocco tayari kwa mchezo wa marudiano utakaofanyika
Jumamosi ijayo jijini Marrakech.
Wenyeji Morocco katika kuhakikisha hawapotezi
mchezo huo, kocha wao Rachid Taoussi ameita kikosi cha wachezaji 24 kati
yao 16 ni wale