Mshambuliaji wa Simba aliyekatisha mkataba wake, Abdalah Juma
amesema msimu ujao ataichezea timu yoyote ya ligi daraja la kwanza na
siyo Ligi Kuu tena.
Juma amesisitiza zipo timu nyingi zilizoonyesha
kumhitaji kwa sasa, lakini ameamua kupumzika kucheza Ligi Kuu na msimu
ujao atatafuta timu ya kuchezea katika ligi daraja la kwanza.
Akizungumza na mtandao huu jana, Juma alisema tayari
amemalizana na uongozi wa Simba na kukabidhiwa barua ya maridhiano ya
kukatisha mkataba.
“Nimemalizana na Simba na wakati wowote
nitatangaza ni timu gani ya daraja la kwanza nitacheza msimu
ujao,”alisema mshambuliaji huyo.