UONGOZI wa timu ya soka ya Ashanti United ya
jijini Dar es Salaam, umesema kuwa haupo tayari kuwapokea na kuwapa
mkataba wachezaji wanaodaiwa kutemwa katika kikosi cha Simba kutokana na
utovu wa nidhamu.
Hivi karibuni kumekuwapo na tetesi za wachezaji
hao wa Simba ambao ni Juma Nyoso, Ramadhan Chombo ‘Redondo,’ pamoja na
Amir Maftah kuhusishwa kutaka kujiunga na Ashanti United kwa ajili ya
kuitumikia katika michuano ya Ligi Kuu msimu ujao.
Katibu Mkuu wa Ashanti United, Abubakari Siyas
alisema jana kuwa, timu hiyo siyo kituo cha tiba kwa watovu wa nidhamu
hivyo wachezaji hao hawana nafasi ya kuitumikia klabu hiyo. Alisema sera
ya Ashanti United siku zote ni kutumia wachezaji wa ridhaa wenye
nidhamu na moyo wa kujitolea