BAADA ya Meya wa Verona kusema Ijumaa
kwamba Mario Balotelli anajitakia mwenyewe matatizo ya kuzomewa,
mshambuliaji huyo wa AC Milan alifanya kituko kingine baada ya timu yake
kuchapwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza wa Serie A.
Mashabiki wa timu wenyeji walimzomea
mshambuliaji huyo wa Milan huku wakitaja jina lake, Balotelli akaa chini
uwanjani mwishoni mwa mchezo, akishuhudia mashabiki wa timu hozo mbili
wakitupiana viti.
Mshambuliaji mkongwe, Luca Toni
aliisaidia Hellas Verona kutoka nyuma kwa bao moja na kushinda dhidi ya
Milan katika mchezo wao wa kwanza Serie A baada ya miaka 11.
Majanga: Mario Balotelli akiwa amekaa uwanjani baada ya Milan kulala 2-1 mbele ya Hellas Verona
Mawili: Mshambuliaji mkongwe Luca Toni amefunga mabao mawili
Bao la kichwa lililofungwa na mwanasoka
huyo wa zamani wa kimataifa wa Italia dakika ya 29 na lingine dakika ya
53 yaliihakikishia pointi tatu Verona.
Milan ilicheza ovyo licha ya kutangulia kupata bao dakika ya 14 kupitia kwa Andrea Poli.
Kiatu: Meya wa Verona, Flavio Tosi amemuitwa Balotelli msababisha matatizo kwenye mechi