“Siwezi kumwangusha Rais Jakaya Kikwete, namwahidi
nitashinda mchezo wa leo na kuubakisha mkanda wa ubingwa Tanzania,”
alisema Cheka wakati akiongea na jana.
Cheka anashuka ulingoni, Diamond
Jubilee kuzikunja na Williams katika pambano la kuwania Ubingwa wa
Dunia (WBF), huku Makamu wa Rais, Gharib Bilal akiwa mgeni rasmi
kumwakilisha Kikwete.
Mabondia hao, jana walipima uzito jijini Dar es
Salaam tayari kwa pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na
mashabiki wa ndondi nchini.
“Najua JK (Jakaya Kikwete) ni mpenda michezo na
anatoa sapoti kwenye michezo, hivyo namwahidi kufanya kweli leo,”
alisema Cheka na kuongeza: “Nimejipanga kushinda pambano hili,
nilishasema tangu awali, narudia kusema tena, sitawaangusha mashabiki
wangu.”
Aliongeza: “Niko tayari kufia uwanjani, lakini siyo kuliona taji linaondoka Tanzania. Nitamaliza kazi kwa mafanikio.
Kwa upande wake, Williams alisema amekuja
kushindana na siyo kinyume chake, hivyo anajiandaa kutoa upinzan mkali
dhidi ya mpinzani wake.
Mwanamasumbwi huyo anashuka dimbani ikiwa ni wiki mbili kupita tangu amshinde kwa pointi bondia wa Malawi,
Chiotcha Chimwemwe. Pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi kati ya
Thomas Mashali na Mada Maugo watakaowania Ubingwa wa WBF Afrika.