come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

KOCHA YANGA ATABIRI USHINDI KWA YANGA DHIDI YA AZAM JUMAMOSI



WAKATI kikosi cha Azam FC kikitarajiwa kuwasili nchini leo kutokea Afrika Kusini, Kocha Mkuu wa Yanga Ernie Brandts (Pichani), amesema mechi ya Ngao ya Jamii dhidi yao Jumamosi itakuwa ngumu kutokana na upinzani ulioko baina yao.

Azam FC, iliweka kambi ya siku 12 nchini humo huku ikicheza mechi nne za majaribio na kupoteza tatu dhidi ya Moroka Swallows jana 1-0, Orlando Pirates 2-1, Kaizer Chiefs 3-0 na kuishinda Mamelodi Sundowns 1-0.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Sports Club Villa ya Uganda na Yanga kushinda 4-1, Brandts alisema, mchezo huo ulikuwa mzuri kwao na umempa nafasi ya kujua penye tatizo ili aweze kulifanyia kazi kabla ya kuwakabili Azam Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, ikiwa ni mchezo wa kuashiria kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom.

Brandts, licha ya timu yake kushinda katika mchezo wa juzi, alikiri uwezo wa Azam FC ni mkubwa na kuwa Jumamosi atakayemzidi mbinu mwenzake ndiye atakayeshinda, japokuwa ana imani kubwa na kikosi chake.

“Katika timu ambazo zina changamoto kubwa katika soka la Tanzania ni Azam FC na mchezo wa Jumamosi lolote linaweza kutokea, kwani sisi ni wazuri hata Azam FC nao ni wazuri pia, kwa hiyo mshindi atajulikana siku hiyo,” alisema Brandts.