|
|
Hatima ya mwalimu mwenye asili ya Ubelgiji, Luc Eymael, katika
miamba wa Ligi Kuu Kenya, AFC Leopards haijulikani baada ya kocha huyo
kuripotiwa aliondoka nchini bila idhini.
Nicholas Muyoti ameteuliwa na kamati tawala ya klabu hicho kama mwalimu wa muda huku akipewa kibali cha kutayarisha wachezaji kwa mechi yao ya wikendi hii.
Katibu mkuu wa Leopards, George Aladwa, alidokezea SuperSport.com kutorithika kwake na hatua hiyo ya kocha.
“Eymael aliasi jukumu lake na kuondoka hapa nchini bila ruhusa wala kutujuza. Imekuwa wiki moja sasa tangu tulipomuona mara ya mwisho. Tumetatanishwa sana na kitendo chake nah ii ni kumuarifu kwamba klabu kitachukua hatua za kinidhamu dhidi yake na atakaporejea, tutajadili mwelekeo,” Aladwa alisema.
Eymael amekuwa akishinikiza aongezewe mshahara baada ya kuongoza Leopards kupanda kutoka nafasi ya 13 hadi ya tatu katika msururu wa ligi huko akidokeza ana fursa bora zaidi mahala pengine.