come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

NGASSA ALIA KUIKOSA AZAM, ADAI AMEONEWA

Kiungo mshambuliaji wa mabingwa wa soka nchini Yanga, Mrisho Ngassa (Pichani) amemwaga chozi asubuhi ya leo baada ya kuikosa mechi ya kukata na shoka kati ya timu yake ya sasa Yanga na ile ya zamani Azam ambayo itapigwa jioni ya leo kuwania Ngao ya Jamii.


Akizungumza na mtandao huu, Ngassa amesema kitendo cha kufungiwa na TFF kwa kusajili timu mbili kimemuuma sana na kwa hilo anamuachia mungu, anasema kuwa yeye hajawahi kusaini mkataba wowote wa nyongeza na Simba na alikuwa akilishangaa suala hilo kupitia vyombo vya habari.

Ngassa ameongeza kuwa kama maamuzi yametoka na yeye amefungiwa basi anamuachia m7ungu lakini kwa dini yake ya Kiislamu hakuwahi kufanya hivyo, Kuukosa mchezo wa leo ni dhambi kubwa kwake kwani alitaka awemo katika kikosi cha kwanza ili awaonyeshe soka vijana wa Azam amvbao wamechangia matatizo yake yoye ya kumpeleka Simba kwa mkopo.

Amedai kuwa atatoa tamko kamili hivi karibuni kuhusu kukubali kuilipa Simba au kukataa na kutaka suala hilo lipelekwqe sehemu nyingine za sheria ili haki yake iweze kupatikana, 'Kwa sasa siwezi kulizungumzia hilo bado mapema ila subiri nitasema', alisema Ngassa.

Jana kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ilimidhinisha Ngassa kuichezea Yanga msimu ujao unaoanza leo lakini ikimtaka ailipe kwanza Simba shiligni milioni 45 pamoja na adhabu ya kusimama mechi sita