Mcheza kiungo wa klabu ya Queen Park Rangers Stephane Mbia (Pichani), amejiunga na klabu ya Sevilla kwa mkopo.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Cameroon, mwenye umri wa miaka 27, sasa ataichezea klabu hiyo ya Uhispania msimu huu wote.
Mbia alijiunga na QPR, kutoka klabu ya Marseille mwaka uliopita, kwa mkataba wa miaka miwili, naye Joey Barton akajiunga na Marseille msimu huo kwa mkopo.
Aliicheza QPR mechi 32, ishirini na nne wakati klabu hiyo iliposhushwa daraja msimu uliopita.
Mbia ni mchezaji wa Saba kukihama klabu hiyo ya Rangers, kwa mkopo au kwa mkataba wa kudumu tangu waliposhushwa daraja.
Katika miezi ya hivi karibuni, klabu hiyo imepoteza wachezaji wake Christopher Samba, Djibril Cisse, Jose Bosingwa, Loic Remy, Esteban Granero na Park Ji-sung.
Mchezaji huyo kutoka Cameroon, alipigwa faini na QPR mwezi Mei mwaka uliopita, wakati alipotuma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter akiashiria kuwa anataka kurejea Uhispania na kuichezea klabu yake ya zamani