come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

TUSKER YABANWA MBAVU NA THIKA UNITED LIGI KUU KENYA

Francis Kahata

Mabingwa Tusker walitoka bao moja nyuma na kutoka sare ya bao moja moja na Thika United katika pambano la kuvutia lililochezewa uga wa City Jumapili adhuhuri.
Mechi hiyo iliyokuwa na kasi sana ilianza huku timu zote zikionyesha nia ya kutoroka na alama zote na ni Thika waliobahatika kwanza dakika ya 25 kupitia bao lililofanyiwa kazi sana.
Wycliffe Opondo na Francis Kahata walibadilishana pasi za kipekee za moja mbili kabla ya Kahata kumalizia kwa kombora la chini kwa guu la kulia ambalo lilimpita kipa wa Tusker Samuel Odhiambo na kuwapa vijana hao wa Brookeside uongozi.
Baada ya kuwa nambari mbili kwa mchezo kwa muda, kocha wa Tusker Robert Matano alifanya mabadiliko mapema kipindi cha pili na kuingiza Robert Omunuk na Victor Ali Abondo; hatua ambayo ilitia nguvu kikosi chake na wakaanza kushambulia.
Presha hatimaye ilizaa matunda dakika ya 52 pale mpira ulioandaliwa na Abou Omar ulipofungwa kwa kichwa na mfungaji mabao bora wao Jesse Were kipa wa Thika Lucas Indeche akibaki bila la kufanya na mabao yakawa 1-1.
Tusker walikuwa na fursa ya kushinda karibu na mwisho wa mechi lakini kombora la Omunuk likafagiliwa na Tony Kizito baada ya kosa la Indeche huku Were naye akikaribia kufunga kwa kichwa tena baada ya kuandaliwa mpira na Athman Buki.
Baada ya mechi hiyo, kocha wa Thika John Kamau alidokezea supersport.com kwamba aliridhishwa na matokeo.
“Nimeridhika na matokeo na mchezo wa wachezaji wangu. Ilikuwa ni mechi nguvu lakini tulionyesha Tusker kwamba sisi si wachache kwani tuliwakabili kila waliposhambulia na kujaribu ujanja wao.”