come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MBIO ZA SOWETO MARATHON MATATANI KUFANYIKA

Soweto ni mji wa mabanda unaosifika Afrika Kusini
Ugomvi umeibuka baina ya watayarishaji wa mbio za Soweto Marathon wakisema mbio hizo hazitofanyika tarehe 3 Novemba huku James Evans rais wa shirikisho la riadha Afrika Kusini akisema mbio hizo zitaendelea kama ilivyopangwa.

Vijana wa Soweto Marathon Trust walioanzisha mbio hizo wamesema kuna wasiwasi kuwa bwana James Enas huenda akazipeleka mbio hizo mjini Cape Town anakotokea lakini kamwe hazitofanyika eneo la Soweto.
Wanamlaumu James Evans kwa kutumia pesa za kuandaa mbio hizo kwa mambo mengine na pia Bwana Evans hataki kusema kiasi gani wafadhili walichotoa.
Hata hivyo James Evans ansema kuwa baadhi ya ripoti zinazosema kuwa mbio hizo zimefutiliwa mbali na Soweto Marathon trust ni sehemu njama ya kutaka kumng'oa madarakani.
Mfuko huo wa Soweto Marathon Trust unahitaji dola mia 5 elfu kuandaa mashindano hayo yaliyoanzishwa mwaka 1991 yakiwa maarufu kupita yote barani Afrika.
Mshindi wa mbio hizo mwaka jana alikua Shadrack Kemboi wa Kenya. Sasa Soweto Marathon Trust wanamtaka waziri wa Michezo wa Afrika Kusini Fikile Mbalula (Vuvuzela ) aingilie kati.