Rafael Nadal amemcharaza bingwa
wa dunia wa tennis ya wanaume Novak Djokovic kwenye mchuano wa fainali
ya shindano la US open mjini New York Marekani na ambalo amelishinda kwa
mara ya pili.
Mchuano huo wa seti nne ulikuwa mkali sana.
Nadal raia wa Uhispania na mwenye umri wa miaka 27, alicheza vyema sana na kushinda mchuano kwa 6-2 3-6 6-4 6-1 katika muda wa saa tatu na dakika ishirini na moja.
Nadal sasa ameshinda mashindano 13 makubwa ya Grand Slam na kusemekana kuwa mchezaji pekee anayeweza kumkaribia aliyekuwa bingwa wa tennis Pete Sampras.
Na baada ya kukosa kushiriki michuano ya US Open mwaka jana kutokana na jeraha, Nadal sasa anajiandaa kuchukua nafasi ya kuwa mchezaji nambari moja wa Tennis duniani.
"ushindi wangu umenifurahisha sana,'' alisema Nadal akiongeza kuwa hakutarajia kushinda. ''Hivyo ndivyo maisha yalivyo, na nina bahati sana.''
"napenda sana ushindani na pia napenda sana mchezo huu. Maisha yangu yote nimekuwa nikiota kuhusika na mashindano kama haya.