Staa wa muziki wa kizazi kipya nchini maarufu bongofleva Nasibu Abdulmaliki 'Diamond Plutinum' (Pichani) amemtaka mwanamuziki mwenzake wa muziki huo Dayna kuacha kutafuta umaarufu kupitia mgongo wake kwa madai ya kuibiwa wimbo wake.
Diamond ameyasema hayo hivi karibuni ambapo amedai anashangaa kuhusishwa katika wizi wa nyimbo ya Dayna wakati si kweli kama yeye amemuibia, ameongeza kuwa yeye alikwenda kwenye studio za Burn Record kwa lengo la kurekodi wimbo wake mpya Number One ambalo ni wazo lake binafsi na wala si kuiba au kukopi.
Anaongeza kuwa alipofika studio alisikilizishwa hala nyingi yaani (beats) na prodyuza ikiwemo hala ya wimbo wa Number One, baadaye akaridhishwa na hala ya wimbo wa Number One na kuamua kuichukua na kuwa ya kwake.
Prodyuza wa nyimbo hiyo Sheddy Clever alimkubali kuichukua hala hiyo na kuanza kuingiza sauti (vocal) baadaye akaiweka hadharani ambapo anashangaa kusikia taarifa hizo kuwa ameiba wimbo wa Dayna kitendo ambacho kinamwaribia sifa yake ndani na nje ya nchi.
Kwa sasa Diamond anaitangaza vema nchi kutokana na kazi zake kukubalika kimataifa kitendo cha kumuhusisha na wizi wa nyimbo hakikubaliki hata kidogo, Dayna ametakiwa kujituma na ipo siku mwenyezi mungu atamnyooshea njia na kufanikiwa kama ilivyo kwa wanamuziki wengine