come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

SIMON MSUVA AMPOTEZA NGASA YANGA

Kasi ya uchezaji ya kiungo mshambuliaji Simon Msuva imeonyesha matumaini ya hali ya juu na kusababisha wapenzi na mashabiki wa Yanga kumsahahu kwa muda Mrisho Ngasa ambaye amesimamishwa mechi sita na TFF.


Kwa mujibu wa mashabiki wa Yanga wanaojitokeza kwenye uwanja wa Taifa kushuhudia mechi mbalimbali wamedai kasi ya Msuva inawapa matumaini makubwa na wala hawana haja na Ngasa ambaye bado anaendelea na dhabu.

Pia kocha wa Azam Mwingereza Stewart Hall ameonyesha kutishwa na kasi ya Msuva na kudai Yanga imepata bonge la kiungo mshambuliaji, amedai uchezaji wa Msuva umechangia timu yake kucheza kwa taadhali kubwa wakati ilipokutana na Yanga.

Naye Msuva amesema kwamba mikakati yake ni kulinda nafasi yake ili aendelee kuisaidia Yanga katika mbio za kusaka ubingwa wa bara msimu huu, Msuva amecheza vizuri karibu mechi zote alizopangwa na kusababishwa Wanayanga kutokuwa na hamu ya kumuona Ngasa akiichezea timu hiyo, Yanga itashuka jumapili kuivaa Ruvu Shooting ya Pwani