Habari tulizozipata zinasema kuwa gwiji la sanaa za vichekesho nchini, Amri Athumani 'King Majuto' ametangaza kugombea ubunge kwa 2015.
Muigizaji huyu mkongwe mzee Majuto ametangaza kugombea ubunge jimbo la Tanga mjini.
Majuto mwenye umri zaidi ya miaka 60 ametangaza nia yake hiyo alipohojiwa na Clouds, na akadai atagombea kupitia CCM.
Bado tunamtafuta mzee majuto ili aweze kututhibitishia kama habari hizi ni za kweli au la na kama ni kweli ana mipango gani na jimbo hilo la Tanga mjini.
Lakini jana alithibitisha kuwa anayo mipango hiyo ya kugombea ubunge kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Majuto ni mmoja kati ya wasanii wanaotesa kwa fedha kwa sasa hapa nchini