come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

GARETH BALE AMTISHIA NYAU RONALDO.

WINGA Gareth Bale amesema kwamba kwa sasa yuko fiti kabisa baada ya mwanzo mgumu katika kabu yake mpya, Real Madrid na sasa yuko tayari kuwafanyia mambo mazuri vigogo hao wa Hispania.

Miezi miwili ya mwanzo ya nyota huyo wa Wales miguu yake ilikuwa migumu Hispania tangu asajiliwe kutoka Tottenham ya England Septemba 1 kutokana na kuandamwa na majeruhi.

Bale aliumia mara mbili katika mwezi wake wa kwanza, lakini ameweza kufunga mabao matatu hadi sasa na kusababisha mabao matano kwa Los Blancos, ambayo inashika nafasi ya tatu kwa ssa katika La Liga na kuongoza kundi lake katika Ligi ya Mabingwa.