come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

GEORGE WAKUGANDA AMPA JINA MTOTO IVO MAPUNDA

Mkurugenzi wa kampuni inayojihusisha na masuala ya michezo ya Smart Sport yenye maskazi yake jijini Dar es Salaam George Michael Wakuganda (Pichani) ambaye pia ni muandaaji wa mechi za kirafiki zinazoihusisha klabu za Yanga na Simba amempachika jina mtoto wa mdau maarufu wa soka nchini Prince Hoza ambaye naye ni mkurugenzi wa Mambo Uwanjani Publishers Prince Hoza.

Wakuganda ameandika katika ukurasa wake wa facebook kuwa anapendelea mtoto huyo aitwe jina la Ivo Mapunda kwa vile alizaliwa siku ambayo Ivo Mapunda aliiokoa Tanzania wakati akicheza penalti mbili wakati timu ya taifa ya Tanzania bara ilipoichapa Uganda kwa mikwaju minne ya penalti dhidi ya mitatu ya Uganda.

Hoza alijaaliwa kupata mtoto kupitia kwa mke wake ambaye alijifungua siku ya Jumamosi ambapo Stars ilicheza na kuibuka na ushindi, 'Ni kweli mke wangu alijifungua siku ya Jumamosi ambayo Stars ilishinda na muda ni ule ule, kuna kipindi niliwaza kumpa jina hilo la Ivo', alisema na kuongeza Hoza.

'Nashukuru Wakuganda amenichagulia jina la kumpa bila shaka nitampa jina hilo, kwanza limetolewa na mwanamichezo mashuhuri hapa nchini najivunia pia mwanangu kupewa jina la shujaa wa Tanzania isitoshe aliyebuni ni mdau mkubwa', aliendelea.


Aidha Hoza amedai kuwa mtoto huyo alizaliwa nje ya Dar es Salaam na yeye yupo jijini Dar itambidi asafiri hadi alipo mtoto Morogoro ambapo ndipo alipozaliwa, Hoza amedai atakwenda huko Jumamosi na atamweka hadharani mwanaye.