come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

HAYATI MANDELA AENDELEA KUMIMINIWA SIFA.

Mwili wa hayati Nelson Mandela umewekwa katika jengo la Union ambako aliapishwa wakati aliingia mamlakani mwaka 1994.

Jeneza lake likiwa limefunikwa bendera ya taifa , lilipitishwa kwa umma likisindikizwa na msafara wa magari na pikipiki.

Wanajeshi waliobeba jeneza hilo walisonga hatua kwa hatua hadi katika Majengo ya union eneo alikoapishwa kuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika kusini 1994.


Mwili huo sasa utaweza kutizamwa na wageni mashuhuri pamoja na wananchi wa kawaida.

Wageni hata hivyo hawaruhusiwa kupiga picha.

Mwili wa Mandela utawekwa katika hali hiyo kwa siku tatu zijazo hadi atakapozikwa Jumapili.

Leo jioni wasanii mbali mbali wa Afrika Kusini watashiriki katika tamasha maalum la kumuenzi Mandela na ambalo wananchi wataruhusiwa kuhudhuria bila malipo.