KLABU ya Manchester City imewafunga mabingwa wa Ulaya Bayern Munich mabao 3-2 Uwanja wa Allianz Arena, Munich katika mchezo wa Kundi D, Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Thomas
Muller alitangulia kuwafungia wenyeji bao dakika ya tano, pasi ya ,
Dante na Mario Gotze akafunga lpili dakika ya 12, kabla ya City kuanza
safari ya kupanda mlima hadi kuibuka na ushindi huo.
David
Silva alifunga la kwanza dakika ya 28 pasi ya James Milner na Kolarov
akafunga la kusawazisha dakika ya 59 kabla ya Milner kufunga la ushindi
dakika ya 62, pasi ya Jesus Navas.
Kwa
ushindi huo, City imetimiza pointi 15 sawa na Bayern baada ya kucheza
mechi sita, lakini mabingwa wa Ulaya wanaendelea kukaa kileleni mwa
Kundi D, kutokana na wastani wao mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
James Milner alifunga mabao mawili City ikiilaza 3-2 Bayern
Bayern inaendelea kuongoza Kundi D kwa wastani mzuri wa mabao
Kocha Pellegrini alimtoa Edin Dzeko dakika za mwishoni