come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

TEGETE AAPA KUWATUNGUA BERKO, MAPUNDA.

MSHAMBULIAJI wa Yanga Jerryson Tegete ambaye amekuwa na historia nzuri ya kuifunga Simba amesema endapo atapangwa katika kikosi cha kwanza siku ya Jumamosi watakapoivaa Simba katika mechi ya 'Nani mtani Jembe' kwenye uwanja wa Taifa ataifunga tena timu hiyo.

Tegete ameyasema hayo alipozungumza na STAA WA LEO ambapo amedai kuwa anawajua vema makipa Ivo Mapunda na Yaw Berko ambao kwa sasa wamesajiliwa na Simba, 'Berko au Mapunda lazima nimtungue, hawa jamaa nawafahamu vema nimecheza nao Yanga kwa vipindi tofauti najua udhaifu wao', alisema Tegete.


Aidha mshambuliaji huyo anaomba dua ili kocha wake Ernie Brandts amwanzishe katika kikosi cha kwanza ili kutimiza azma yake hiyo, mshambuliaji huyo kwa sasa amekutana na changamoto nyingi zinazopelekea kukaa benchi hasa baada ya kuwepo kwa washambuliaji sita katika kikosi hicho.


Washambuliaji hao ni Hamisi Kiiza, Hussein Javu, Said Bahanuzi, Shaaban Kondo, Didier Kavumbagu na chipukizi Reliant Lusajo, pia kusajiliwa kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi kunaweza kumpoteza kabisa straika huyo aliyevuma enzi ya Mbrazil Marcio Maximo.