come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

RAGE AWASHUSHIA ZIGO LA OKWI HANSPOPPE, KABURU.

MWENYEKITI wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage amewabebesha zigo la mshambuliaji Emmanuel Okwi mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo Zackaria Hanspoppe na aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange 'Kaburu'.

Akizungumza hiuvi karibuni Rage amesema kwamba yeye pekee si wa kupewa lawama kuhusu mauzo ya Okwi katika klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia na kupelekea kutolipwa fedha zao kwa wakati, Rage ameyasema hayo kufuatia lawama zinazotolewa na wanachama, wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo kudai kuwa amekula fedha za usajili wa Okwi.

Rage amekataa katukatu kuwa yeye hajala hata kidogo fedha za Okwi ila anachofahamu klabu ya Simba inaidai Etoile Du Sahel fedha za usajili wa Okwi ambazo ni milioni mia nne, Aidha mwenyekiti huyo amewataka mashabiki na wanachama wa Simba kutomsakama yeye peke yake isipokuwa wafanye hivyo kwa Kaburu na Hanspoppe kwani na wao wanahusika.


Rage ameendelea kudai kwamba kuna kikundi kinachojiita wapenda Simba wamepanga kwenda nyumbani kwake ili kumshinikiza ajiuzuru na kueleza kwa kina zilizpo fedha za Okwi, Rage amewashangaa watu hao wanakumbuka sasa kutaka kwenda kwake wakati sakata la Okwi lilianza tangia mwezi April mwaka huu.

Aidha mwenyekiti huyo amewaambia Wanasimba kuwa Okwi si mali ya Simba tena kwani aliuzwa kihalali kwa klabu ya Etoile Du Sahel isipokuwa wanaidai fedha za mauzo hayo, Okwi kuichezea Yanga si tatizo na wala awezi kuipoteza Simba.