come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

YANGA YANASA STRAIKA HATARI WA BURUNDI.

Kamati ya usajili ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Yanga, imewasili jijini hapa jana kwa ajili ya kusaka wachezaji mbalimbali wa kuwasajili kupitia michuano ya Kombe la Chalenji inayoendelea nchini Kenya.

Licha ya kamati hiyo kutokuwa tayari kuweka wazi ni nyota gani wamewavutia, habari kutoka chanzo chetu cha ndani zimeeleza kuwa, wamevutiwa na kiungo mshambuliaji wa Burundi, Fiston Abduol.

Yanga mwakani inatarajia kushiriki katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu Kombe la Kagame.


Akizungumza na mtandao huu, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Abdallah Binkleb, alisema walianza kuifuatilia michuano hiyo kupitia televisheni wakiwa nchini Tanzania na sasa wanataka kujiridhisha kwa jana kuishuhudia mechi kati ya timu ya Bara (Kilimanjaro Stars) dhidi ya Burundi.

Mchezaji mwingine ambaye ameonyesha kiwango cha juu katika mashindano haya yanayotarajiwa kumalizika Desemba 12 ni Danny Sserunkuma, ambaye anaichezea klabu ya Gor Mahia ya Kenya.

"Tumekuja pia kuangalia timu yetu ya Tanzania Bara," alisema kwa kifupi Binkleb ambaye ameambatana na Seif Ahmed, mjumbe wa kamati hiyo.

Aliongeza kuwa, Yanga imekuwa makini katika usajili wake mwaka huu kwa sababu imejipanga kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa mwakani na kuhakikisha wanatetea ubingwa wao wa Bara.

Nyota wengine wawili wa Yanga wanaocheza katika mashindano haya ni Hamis Kizza ambaye yuko na Uganda Cranes, wakati Haruna Niyonzima ndiye nahodha wa kikosi cha Rwanda (Amavubi).