come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

YANGA WALIA NA HUJUMA ZA TFF KUHUSU OKWI.

Uongozi wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, Yanga, umesema Shirikisho la Soka nchini (TFF), linawahujumu kuhusu suala la mshambuliaji wao Emmanuel Okwi aliyesimamishwa kuitumikia klabu hiyo katika mechi za Ligi Kuu.

Lakini ukafafanua kwamba haujakaa kimya bali unaendelea kulifanyia kazi suala la kusimamishwa kwake.

Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Usajili ya Yanga, Abdallah Binkleb, alisema wanaamini kuna ‘hila’ zimefanyika dhidi ya klabu yao na mwisho wa tatizo hilo utajulikana hivi karibuni.

Binkleb alisema Yanga ilifuata taratibu zote katika usajili wa mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba, lakini wameshangazwa na maamuzi ya kumsimamisha yaliyotolewa na TFF siku chache kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi.

“Hatujakaa kimya, kuna vitu tunavifanyika kazi na kati ya leo (jana) jioni na kesho (leo) tunaweza kuvikamilisha, hatuko kimya tu ila tunataka kujiridhisha kwa mara nyingine,” alisema Binkleb.


TFF iliamua kuandika barua katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuomba mwongozo kutokana na kuwapo kwa kesi tatu tofauti zinazomhusisha Okwi.

Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura, aliliambia gazeti hili jana kwamba bado shirikisho hilo halijapokea majibu yoyote kutoka Fifa kama walivyoomba muongozo.

Kutokana na kusimamishwa huko, Okwi ameshakosa kuitumikia Yanga katika mechi mbili za ligi ya kwanza ikiwa ni dhidi ya Ashanti United na jana dhidi ya Coastal Union.

Simba pia imefungua kesi Fifa ikidai malipo yake ya Dola za Marekani 300,000 ambazo hawajalipwa na uongozi wa klabu ya Etoile Sportive du Sahel baada ya kumuuza Mganda huyo.

Okwi alisajiliwa na Yanga katika kipindi cha dirisha dogo Desemba mwaka jana na mechi pekee ya mashindano aliyoichezea Yanga ni ya kuwania Kombe la 'Nani Mtani Jembe' huku akiichezea timu hiyo michezo mingine ya kirafiki ambayo klabu hiyo ilicheza ilipokuwa kambini nchini Uturuki.

Mbali na Okwi, Yanga pia walimsajili Juma Kaseja na kiungo, Hassan Dilunga, ili kuimarisha kikosi chao katika usajili wa dirisha dogo.