Yanga iliyoondoka leo asubuhi, imetua nchini humo ikiwa na matumaini makubwa ya kusonga mbele, baada ya kuichapa Komorozine mabao 7-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam Jumamosi.
Wachezaji wa Yanga kutoka kulia Mrisho Ngassa, Juma Abdul na Haruna Niyonzima wakiwa Comoro. Chini ni Mrisho Ngassa aliyefunga mabao matatu katika ushindi wa 7-0.
Iwapo Yanga itahitimisha vyema kampeni yake hiyo, itakutana na mabingwa watetezi, Al Ahly mwezi ujao.