Akizungumza ajali hiyo katika eneo la tukio Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizunguti alisema basi lao liliacha njia baada ya dereva wao kukwepa kugongana uso kwa uso na basi lingine lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea mikoa ya bara.
“Hii ajali kama siyo akili ya haraka haraka ya dereva wetu kuacha njia na kuseleleka, basi hapa leo kungetokea ajali mbaya tena ingehusisha majeruhi na vifo, lakini tunamshukuru Mwenyezi Mungu hakuna aliyeumia zaidi ya basi kupata mikwaruzo kidogo.”
Kizuguto aliongeza kwa kusema ajali yao imetokana na dereva wa basi lingine aliyekuwa akiyapita malori akiwa katika mwendo kasi na kulazimisha basi la Yanga liachie njia ili basi hilo liweze kupita na endapo isingefanya hivyo, basi hizo zingegongana uso kwa uso.
Malori yalikuwa katika foleni ndefu yakitokea Dar es Salaam kuelekea Morogoro yakielekea mizani ya Mikese, na kutoa nafasi kwa magari yatokayo Morogoro kwenda Dar es Salaam kupita bila kipingamizi.